Sign the Petition

Put early childhood development at the heart of the new post-2015 development framework with targets that promise all children care, support and services which work together for the best start in life.

…We need your support – we need to build alliances to ensure that early childhood development is not just a side issue – it should be right at heart of civil society, our fight for social justice and economic development. We cannot afford to squander the talents of so many of the world’s people.

Sign the petition here: SIGN

Malalamishi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon pamoja na Mataifa Washiriki
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon na Mataifa Washiriki: Toeni kipaombele kwa maendeleo na ukuaji wa watoto wachanga katika mwongozo mpya wa maendeleo wa miaka baada ya 2015. Wekeni shabaha zinazohakikisha utunzaji wa watoto, ufadhili na huduma zitakazowezesha kuwa kwa mwanzo bora wa maisha.

Malalamishi ya Tessa Jowell, London, Uingereza.

Zidisha athari yako

Zidisha uwezo wa sahihi yako kwa kueneza malalamishi haya na kuwaleta watu unaowajua kutia sahihi pia.
Tunajua kwamba unachangia pakubwa katika maisha ya mtoto kwa kuwekeza katika miaka ya kwanza – kutoka utungajimimba hadi miaka tano ya kwanza. Ithibati kutoka kwa mipango kama Sure Start katika taifa la Uingereza, inayoungwa mkono na kile tunachojua kwa sasa kuhusu ukuaji wa akili ya mtoto, inathibitisha manufaa ya kijamii na kiuchumi ya muda mrefu ya sera hii. Naamini kwamba tuna fursa ya kusambaza manufaa hayo kwa watoto maskini zaidi ulimwenguni.

Julai iliyopita nilizuru nchi ya Malawi pamoja na Mbunge kwa jina Ivan Lewis, ambaye pia ni Waziri asiyeteuliwa kirasmi wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza kwa kusudi la kujifunza jinsi mipango ya watoto wachanga inavyoweza kutekelezwa vilivyo katika mataifa yasiyo na rasilimali tulizonazo katika mataifa yaliyostawi, na jinsi mipango hiyo inavyoweza kuwafaidi zaidi watoto wasio na bahati na wanaoishi katika maeneo yaliyotengwa. Ziara hii iliimarisha imani yangu katika kanuni kwamba mtazamo unganifu wa ukuaji wa watoto wachanga utaleta manufaa kamili kwa watoto masikini zaidi pamoja na familia zao.

Tunafanya kazi Uingereza kupitia Kikundi cha wabunge kutoka vyama vyote kilichoundwa na mbunge Andrea Leadsom pamoja na Wabunge kutoka vyama mbalimbali tukilenga kuendeleza mtazamo mseto kuhusu maendeleo na ukuaji wa watoto wachanga. Ikiwa mwongozo mpya wa maendeleo ya miaka baada ya 2015 utakuwa mwongozo wa dhati wa azimio la dunia la ufadhili utakaojumuisha mataifa yanayostawi, yaliyostawi na mataifa yenye mapato ya wastani, tunahitaji kuthibitisha kuwa tunafanya yote tuyawezayo nyumbani ili kupambana na ukosefu wa utoshelevu, umaskini na ukosefu wa nafasi za kujikimu.

Lakini sasa tunahitaji msaada wako – tunahitaji kujenga ushirikiano na mataifa manane tajiri zaidi ulimwenguni (G8) pamoja na mataifa mengine yanayostawi kuhakikisha kwamba maendeleo na ukuaji wa watoto wachanga sio swala la pembeni – linapaswa kuwa swala kuu kwa mashirika ya umma, vita vyetu vya haki ya kijamii na maendeleo ya kiuchumi. Hatuwezi kudidimiza talanta za wengi wa watu wa ulimwengu.

Tusaidie kutafuta uungwaji mkono kwa kusambaza malalamishi haya kwa marafiki zako na wengine wanaoamini kuwa maswala ya watoto yanapaswa kuwa kuu katika mkakati wetu wa maendeleo ya siku zijazo. Ikiwa mwongozo huu ni bora kwa watoto wetu, basi ni bora pia kwa watoto maskini zaidi ulimwenguni. Ndiyo sababu ninaamini sera hii inapaswa kuwa swala kuu katika mwongozo mpya wa miaka baada ya 2015.

Advertisement

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s